Inashauriwa mama anaponyonyesha mwanawe awe amekaa sehemu yenye utulivu isiyo na kelele na amwangalie usoni ili kujenga ukaribu
Maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto kuanzia siku moja hadi miezi sita, hii ni kwa sababu husaidia kumpatia kingamwili, ubongo kukomaa na hata kuwa na afya bora.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Takwimu la Taifa (NBS), mwaka 2015/2016 unaonesha asilimia 97 ya kina mama nchini wananyonyesha watoto wao.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Takwimu la Taifa (NBS), mwaka 2015/2016 unaonesha asilimia 97 ya kina mama nchini wananyonyesha watoto wao.
Hii inadhihirisha kwamba kuna dalili nzuri na mwamko mkubwa wa kina mama kunyonyesha pindi wanapojifungua.
Hata hivyo, licha ya takwimu kuonyonyesha kuwa wananyonesha, bado kunachangamoto kadhaa zinazojitokeza katika aina ya unyonyeshaji.
Miongoni mwa changamoto hizo, zipo zinazosababishwa na mila, desturi, utamaduni na hata uelewa wa jamii kuhusu suala la unyonyeshaji.
Miongoni mwa changamoto hizo, zipo zinazosababishwa na mila, desturi, utamaduni na hata uelewa wa jamii kuhusu suala la unyonyeshaji.
Watoto hawanyonyeshwi kikamilifu
Ofisa wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Lutfrid Nnally, anasema licha ya asilimia kubwa ya kina mama kunyonyesha, wengi wao hawanyonyeshi ipasanyo kama inavyoelekezwa na wahudumu wa afya.
Anasema mtoto anatakiwa anyonyeshwe ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa ili kumpa uwezo wa kunyonya maziwa ya mama, pia kuyafanya yaendelee kutoka vizuri.
“Sasa wanaofuata utaratibu huo ni wachache mno, kati ya watoto kumi, ni watano ndio wanaonyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa, hii inamaanisha kwamba nusu yao hawanyonyeshwi ndani ya hiyo saa,” anaeleza Nnally.
Anasema ni asilimia 53 kati ya 100 ya watoto wanaonyonyeshwa ndani ya hiyo saa moja, jambo ambalo linapaswa wazazi waelimishwe umuhimu wake.
Nnally anasema kuwa mtoto akicheleweshwa kunyonya, maziwa ya mama yanaweza yasitoke kwa sababu yanakuwa hayaendelei kutengenezwa.
“Maziwa hayawezi kutengenezwa mtoto asiponyonya, mama akichelewa kunyonyesha na maziwa yanachelewa kutoka. Kina mama wengi wasiojifungulia kituo cha afya ndio wanaoongoza kwa kutozingatia muda sahihi wa kunyonyesha,” anasema.
Kwa mujibu wa Nnally, asilimia 58 ya watoto wachanga hawanyonyeshwi ipasavyo ndani ya miezi sita, licha ya mzazi kusisitizwa kwamba hapaswi kumpa mtoto kitu chochote isipokuwa maziwa yake.
Kwa mujibu wa Nnally, asilimia 58 ya watoto wachanga hawanyonyeshwi ipasavyo ndani ya miezi sita, licha ya mzazi kusisitizwa kwamba hapaswi kumpa mtoto kitu chochote isipokuwa maziwa yake.
Anasema huwaanzisha chakula mapema hali inayosababisha kupata madhara kiafya.
“Kipindi cha miezi sita mtoto anatakiwa apewe maziwa ya mama pekee, lakini takwimu zilizofanywa na taasisi yetu kushirikiana na NBS inaonesha asilimia 58 ya watoto hawanyonyeshwi ipasavyo.
“Shida hii ipo katika maeneo yote, mjini na vijijni. Watoto wengi wanaanzishwa chakula kabla ya wakati na kuharibu afya zao,” anabainisha Nnally.
“Shida hii ipo katika maeneo yote, mjini na vijijni. Watoto wengi wanaanzishwa chakula kabla ya wakati na kuharibu afya zao,” anabainisha Nnally.
Athari Kutonyonyesha kikamilifu
Nnally anasema katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo, mfumo wa chakula wa mtoto unakuwa bado mchanga, hauna uwezo wa kusaga chakula.
Anasema maziwa ya mama pekee ndio yenye uwezo wa kumeng’enywa, pia yanavirutubisho vya kutosha kwaajili ya kulinda mwili wake.
“Vyakula vingine havina virutubisho vya kutosha ambavyo vipo katika maziwa ya mama, maziwa ya mama pekee ndio yenye kinga mwili kwa hiyo ukimnyima maziwa ya kutosha lazima ataanza kuugua mara kwa mara.

“Anaweza akapata kichomi na kuna uwezekano wa kupata alergy (mzio), tatizo la mfumo wa hewa (pumu), kuharisha na nimonia, mara nyingi maradhi haya huwapata watoto wasionyonyeshwa ipasavyo,” anabainisha Nnally.
Faida za kunyonyesha kikamilifu
Anasema kunafaida nyingi za kiafya anazopata mtoto pindi anaponyonyeshwa kikamilifu.
Mojawapo ni kumsaidia kupata kinga mwilini, pia kukua haraka kwa ubongo hali inayofanya atambue kwa haraka vitu mbalimbali.
Mojawapo ni kumsaidia kupata kinga mwilini, pia kukua haraka kwa ubongo hali inayofanya atambue kwa haraka vitu mbalimbali.
Anaeleza kuwa watoto wanaonyonya ipasavyo huwa wanakua vizuri na ni wachangamfu, tofauti na wasionyonyeshwa ipasavyo.
“Maziwa ya mama yana virutubisho vya kila aina hasa vitamini A ambayo humsaidia kukua akiwa na afya njema na kuepuka magonjwa kwa sababu ya kinga iliyopo,” anasema.
Changamoto za unyonyeshaji
Mgawanyo wa kazi katika jamii unatajwa kuwa changamoto kubwa kwa wanawake wanapokuwa katika kipindi cha uzazi.
Likizo ya wazazi kwa wale wasio kuwa katika sekta rasmi imekuwa kikwazo kikubwa na hivyo kushindwa kunyonyesha kikamilifu.
Likizo ya wazazi kwa wale wasio kuwa katika sekta rasmi imekuwa kikwazo kikubwa na hivyo kushindwa kunyonyesha kikamilifu.
Anasema asilimia kubwa ya wanawake hawafanyi kazi katika sekta rasmi kwahiyo hupata muda mfupi wa kupumzika baada ya kujifungua.
“Licha ya serikali kutoa likizo ya uzazi kwa wanawake waliopo katika sekta rasmi, tatizo linakuja kwamba wengi hawapo sekta rasmi – hujishughulisha na biashara au kilimo hivyo hupata nafasi ndogo ya likizo ya uzazi.
“Katika jamii nyingi, mama akishajifungua hupewa likizo ya mwezi mmoja, miwili au mitatu, wachache mno wanaopewa miezi sita kwahiyo, atapewa kulingana na utaratibu wa jamii hiyo baada ya hapo anaendelea na kazi kama kawaida,” anaeleza Nnally.
Nnally anasema zipo mila na desturi ambazo pia ni kikwazo katika unyonyeshaji, ambapo baadhi ya koo huamini kuwa mtoto anapozaliwa anatakiwa kupewa maji, wengine wanasema asitumie maziwa ya kwanza wakidhani kuwa ni machafu.
“Jamii zingine huwafanyia watoto tiba mbadala kwa kuwalisha au kuwanywesha hili ni tatizo pia. Wanaokataza kumpa mtoto maziwa ya njano yale ya kwanza ni kwamba wanamkosesha mtoto kinga muhimu mwilini, si machafu kama wanavyodhani,” anafafanua Nnally.
Juhudi za uelimishaji
Nnally anaeleza kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatoa elimu kwa jamii kuhusu jinsi ya kunyonyesha kikamilifu na faida zake.
Anasema katika vituo vyote vya afya elimu kuhusu unyonyeshaji inatolewa pindi wazazi wanapoenda kuhudhuria kliniki.
“Baba na mama wakienda kliniki wanapata elimu ya lishe ya mama na mtoto hivyo, elimu inapatikana kila kituo cha afya.
“Wanawake wengi wanaelewa kuhusu unyonyeshaji hivyo, nashauri jamii pindi mama anapojifungua wampe likizo ya miezi sita ili aweze kuhudumia mtoto ipasavyo kwani hakuna mbadala wa maziwa ya mama,” anaeleza Nnally.
Hali ya utapiamlo nchini
Anasema baada ya miezi sita, maziwa ya mama pekee huwa hayamtoshi, anatakiwa kuongezewa vyakula vya ziada vyenye virutubisho vyote.
Kwa mujibu wa Nnally, takwimu zilizotolewa na TFNC mwaka jana, inaonesha hali ya udumavu imepungua kutoka asilimia 50 miaka 10 iliyopita na kufikia asilimia 31.8.
Anasema wanaendelea kufanya juhudi kupunguza idadi hiyo angalau ifikie chini ya asilimia 20. “Miongoni mwa vyakula muhimu kwa mtoto ni pamoja na matunda, mboga za majani, vyakula vyenye asili ya nyama na vingine.

Anasema kwa kipindi hicho mtoto anatakiwa alishwe mara tano kwa siku, changamoto iliyopo ni kwamba wengi hawapewi chakula mchanganyiko.
“Wale wanaopata utapiamlo hawapewi chakula mchanganyiko, mtoto anatakiwa alishwe mara tano kwa siku hadi anapofikisha miaka mitano.
“Changamoto iliyopo mtoto analishwa mara chache, uelewa wa lishe unasababisha udumavu, licha ya vyakula vinavyotakiwa si vya gharama, ni vya kawaida hata shambani vinapatikana, umasikini si tatizo.
“Changamoto iliyopo mtoto analishwa mara chache, uelewa wa lishe unasababisha udumavu, licha ya vyakula vinavyotakiwa si vya gharama, ni vya kawaida hata shambani vinapatikana, umasikini si tatizo.
“Kwa hali ya utapiamlo maeneo ya mjini yanaunafuu kwa sababu kiwango kikubwa cha utapiamlo kipo maeneo ya vijijini,” anabainisha Nnally.
This article was first published by Mtanzania on the link below
https://www.pressreader.com/tanzania/mtanzania/20190801/281792810640171