
Na Sada Amir
Kunyonyesha ni njia ya kuhakikisha mtoto kuanzia siku moja angalau hadi miezi sita anapata chakula (maziwa ya mama) yanayomuwezesha kuishi na kuwa mwenye afya njema.
Chakula cha mtoto mchanga ambacho ni maziwa ya mama hutoa chanzo muhimu cha lishe kwa watoto kabla ya wao kupata uwezo wa kula vyakula vingine kadri wanavyoweza kuendelea kunyonyeshwa.
Kunyonyesha kuna faida nyingi kwa mtoto ikiwemo virutubisho muhimu vinavyokuwa kwenye maziwa ya mama lakini pia upunguza hatari ya vifo vya ghafla kwa watoto wachanga (Sudden infant death syndrome (SIDS) , kunaongeza akili na kupunguza uwezekano wa mtoto kupata magonjwa ya kuambukiza.
Kunyonyesha kuna faida pia kwa mama kwakuwa husaidia uterasi kurejea hali yake ya kawaida kabla ya ujauzito, hupunguza uvujaji wa damu baada ya kuzaa, husaidia uzito wa mama kurudi katika hali yake kabla ya ujauzito, umuimarisha mama kihisia na kupunguza hatari ya kupata kansa ya matiti na kansa ya mfuko wa mayai.
Ili mtoto anyonye maziwa ya mama na kushiba vizuri, lazima akae vizuri kwenye chuchu kwa kuwa akikaa vibaya inampelekea kumeza hewa nyingi, kumsababishia gesi na maumivu tumboni, kupata choo kwa shida na hata kushindwa kupumua kwa mama kumuwekea ziwa lake puani hivyo kumziba pumzi.
Kwamujibu wa muuguzi wa hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo mkoani Mwanza Bertha Yohana anasema ili mtoto akue vizuri, awe na afya njema pamoja na akili ni vizuri anyonye maziwa ya mama pekee bila kupewa kitu chochote tangu kuzaliwa hadi miezi sita baada ya miezi hiyo ndiyo aanze kupewa chakula cha nyongeza.
Bertha anasema ili mtoto anyonye vizuri na kushiba lazima ukaaji wa mtoto uzingatiwe na namna ya kumlaza mtoto wakati wa kunyonya (position) kwakuwa akilazwa vibaya wakati wa kunyonya hewa uingilia kwenye angle za midomo, hivyo mtoto unyonya maziwa na kuvuta hewa kwa wakati mmoja hivyo kupelekea gesi kuingia tumboni.
Anasema, mama amuweke mtoto kiubavu, njia hii inaweza kutumika mama akiwa amekaa huku akiwa amempakata mtoto wake kiubavu au akiwa amelala kiubavu na mtoto akiwa kiubavu (hii hutumiwa hasa na wamama waliojifungua kwa njia ya upasuaji).
Njia ya tumbo kwa tumbo, njia hii tumbo la mama ugusana na la mtoto wakati wa kunyonya huku mkono wa mama wa upande wa ziwa ambao mtoto ananyonya ukiwa umemshika mtoto kama kumsuport .
“Lazima mama azingatie position kwenye kunyonyesha ili mtoto ashibe vizuri, lakini pia kwenye kumnyonyesha hakikisha chuchu yote inakuwa ndani ya mdomo wa mtoto na mtoto mwenyewe awe ametazama kifua cha mama yake (yaani kalazwa kiubavu)”amesema
Muuhudumu wa afya ngazi ya jamii wa Kituo cha Afya Nyanguge Kilichopo wilayani Magu mkoani Mwanza Joyce Nyanda anasema, mtoto akiwa ananyonya mama anatakiwa amshikilie mabegani huku miguu yake ikisapotiwa na mapaja.
Anasema, mtoto anapokuwa ananyonya mama amtengenezee angle kati ya ziwa lake na mtoto alivyokaa, hii inamaanisha mtoto anapokuwa ananyonya asiwe kanyooka, apinde kidogo (akae kiubavu)
“Kuna wamama wengine wanapokuwa wananyonyesha watoto uangalia kwingine na mtoto kaangalia kwingine , lakini kikawaida mama anatakiwa akiwa anamnyonyesha mtoto amtazame maana kuna faida kubwa ikiwemo ya kumjengea mahusiano ya upendo”anasema
Anasema, nivizuri mama ashike chuchu na kuiweka mdomoni kwa mtoto ili anyonye kwakuwa mtoto anakuwa bado ajajua kujihudumia.
Anasema njia nyingine ya kunyonyesha mtoto ni kumbeba mtoto kama kubeba mpira, huku mikono ya mama ikiwa inamshikilia.
Namna ya kujua kama mtoto ameshiba.
Mtoto kutema chuchu, Kwamujibu wa Bertha Yohana mama atajua mtoto ameshiba pale atakapo tena chuchu wakati wa kumnyonyesha au kuacha mdomo wazi.
Mtoto kuanza kufanya vitu vingine, muhudumu wa afya ngazi ya jamii kituo cha Afya Isegeng’he kilichopo halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza Timotheo John anasema njia nyingine ya kujua mtoto ameshiba wakati wa kunyonya nikuanza kufanya shuguli zingine ikiwemo kucheza.
Mtoto kupunguza kasi ya unyonyaji, “njia nyingine rahisi ya mama kujua mtoto wake karidhika au kashiba wakati anamyonyesha ni akiona ile kasi ya kuvuta maziwa inapungua”amesema John
Anasema njia nyingine za kujua mtoto kashibani mtoto kulala usingizi mdomo ukiwa kwenye chuchu, kutokwa jasho, mwili wake kuwa huru na kubeua.
2 Comments
It’s a pity you don’t have a donate button! I’d most certainly donate to this
fantastic blog! I guess for now i’ll settle for book-marking and adding your RSS feed to my Google account.
I look forward to fresh updates and will share this site with my Facebook group.
Talk soon!
My web page 신용카드골드론
Everything is very open with a clear clarification of the issues.
It was definitely informative. Your site is useful.
Thanks for sharing!
Also visit my webpage: 토토사이트