Mimba inapotoka au kuharibika ni dhahiri umpoteza mtoto wakati wa uja uzito. Lakini fikra huwa tofauti kutokana na sababu mbalimbali. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenuni WHO asilimia 10 ya wanawake waliofamahu kuwa wao ni wajawazito hutambua mimba inapoharibika. Hali hiyo hufafanuliwa na kupokelewa kwa namna tofauti ulimwenguni, lakini kwa ujumla mtoto ambaye hufa kabla ya wiki 28 katika ujauzito huwa inasemekana kama upotezaji wa mimba, na watoto wanaokufa baada ya wiki 28 bado ni ujauzito usio riziki. Kila mwaka, watoto milioni 2.6 hawaishi kutokana na mimba kuharibika au kutoka, na vifo vingi kati ya hivyo vinaweza kuzuiliwa linasema shirika la afya duniani. Walakini, kupoteza mtoto au ujauzito usio riziki huwa hauwekei kumbukumbu kwenye mfumo wa usajili wa watoto , hata katika nchi zilizoendelea, na hivyo kudhihirisha kwamba idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi.
Ulimwenguni kote, katika nchi nyingi, hospitali na kliniki mara nyingi hazina rasilimali na waajiriwa wa kutosha. Unyanyapaa, aibu na hatia huwa ni suala la kawaida linalozungumzwa, wanawake ambao wamepoteza watoto wao hufanywa kuhisi kwamba wanapaswa kukaa kimya kuhusu huzuni yao, mara nyingi kwa sababu kupoteza mimba na ujauzito usio riziki bado ni jambo linalochukuliwa kuwa ni la kawaida sana, au kwa sababu linaonekana kwamba haliwezi kuepukika.
Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa kawaida inaaminika kwamba mtotomaliyekufa kabla ya kuzaliwa au kuharibika kwa mimba inatokana na masuala ya uchawi au mashetani.
Haya yote yanasababisha madhara makubwa kwa wanawake. Wengi wanaweza kukabiliana na masuala ya afya ya akili ambayo hudumu kwa miezi au miaka, hata wanapoendelea kuwa na watoto wengine wenye afya.
Larai, ni mfamasia aliye na miaka 44 kutoka Nigeria asimulia alipopoteza mtoto,
“Kukabiliana na hali ya kupoteza ujauzito wa mtoto wangu iliniumiza sana. Wauguzi walichangia sana katika huzuni yangu licha ya mimi pia kuwa ni daktari. Suala lingine ni utamaduni. Katika tamaduni nyingi za Kiafrika, watu hufikiria kwamba unaweza kupoteza mtoto kwa sababu ya laana au uchawi. Hapa, upotezaji wa watoto huwa na unyanyapaa kwa sababu watu wengine wanaamini kuwa mwanamke anayepoteza mtoto mara kwa mara ana nuksi, au laana na pia inawezekana kuwa amekuwa mzinifu hapo awali na kwa hivyo upotezaji wake ujauzito ni kama adhabu kutoka kwa Mungu.”
Source: UN News