Mambo muhimu ya kuzingatia
Ili kuboresha hali yake ya lishe kwa mama anayenyonyesha, anashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo:
- Kula milo kamili zaidi ya mitatu kwa siku, mlo kamili ni mlo wenye chakula mchanganyiko angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la chakula.
- Kula chakula kingi na cha kutoshakatika kila mlo.
- Kula asusa kati ya mlo na mlo.
- Kumeza vidonge vya kuongeza damu (FEFO) kwa kipindi cha miezi 3 baada ya kujifungua.
- Kutumia vyakula vilivyoongezwa virutibishi, kama vile unga wa ngano, unga wa mahindi, mafuta ya kupikia na kutumia chumvi yenye madini joto.
- Kuongeza ulaji wa vyakula vyenye asili ya wanyama mfano nyama, kuku, mayai, maziwa, samaki, dagaa n.k. Vyakula vya asili ya wanyama vina virutubishi vya aina mbalimbali kwa wingi ikiwemo madini chumaambayo husaidia kuongeza damu mwilini.
- Kutumia chumvi yenye madini joto
- Kula matunda ya aina mbali mbali na mbogamboga kwa wingi
- Kunywa maji ya kutosha kila siku (angalau glasi 8 au lita 1.5),.
- Kujikinga na Malaria kwa kulala kwenye vyandarua vilivyowekwa dawa kila siku.
- Kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa na virusi vya UKIMWI
- Source: TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA
- Link: https://www.tfnc.go.tz/tips/lishe-ya-mama-anayenyonyesha