Na Sada Amir
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (Who), Maziwa ya mama ni chakula bora kwa watoto wachanga (Infant) salama, masafi na yanakinga za mwili ambazo husaidia kuwalinda watoto dhidi ya magonjwa yakuambukizwa.
Maziwa ya mama hutoa nguvu na virutubisho vyote ambavyo mtoto mchanga anahitaji kwa miezi ya kwanza ya maisha yake na yanatoa nusu au zaidi ya mahitaji ya lishe ya mtoto wakati wa nusu ya pili ya mwaka wa kwanza wa kuzaliwa hadi theluthi moja wakati wa pili mwaka wa maisha yake.
Katika unyonyeshaji wa mtoto, kuna hatua za unyonyeshaji ambazo mama anatakiwa kuzifuata ili mtoto anyonye vizuri na kushiba bila shida na endapo hatofuata hatu za unyonyshaji anaweza kusababisha hewa kuingia tumboni kwa mtoto na kumsababishia maumivu na kumkosesha furaha.
Daktari wa wanawake hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo Mkoa wa Mwanza Dk Boniface Messanga ametaja baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha hewa kuingia tumboni kwa mtoto wakati akiwa ananyonya kuwa ni mtoto kunyonya huku analia, mama akimuwekea chuchu vibaya, mtoto kutopata choo pia inasababisha hewa kujaa tumboni.
“Mfumo wa chakula wa watoto bado haujakomaa, kwahiyo bado unajifunza kuchakata chakula ili kiende kwenye mfumo wa haja, kwa sababu mfumo haujakomaa ndio sababu pia wakati wa uchakataji wa chakula kutengeneza kinyesi, kunasababisha utengenezaji wa gesi kule ndani. Sasa hiyo ni sababu ambayo haizuiliki, ipo kwa watoto wenyewe,”amesema Dk Messanga
Ametaja mbinu za kumtoa mtoto hewa tumboni baada ya kunyonyesha kuwa ni kusukuma kidogo kidogo tumbo la mtoto/kukandamiza kidogo kidogo kwa kuwa viungo vya mtoto havijakomaa (ku apply pressure), amesema kufanya hivyo kunafanya hewa kutoka tumboni kwa mtoto kuanza kubeua.
Kutumia mpira wa kuchezea (football), “ Unaona katoto kalivyo vili? Mpira na wenyewe sio mgumu sana. Kwahiyo unakalaza mtoto anaulalia kwa tumbo, kwahiyo unakuwa kama unauvilingisha mpira. (ukiuviringisha mpira mtoto atazunguka huku na huku) hiyo ni namna pia nzuri ya kuondoa hewa”amesema Dk Messanga
Mbinu nyingine ni kukanda kanda mtoto mgongoni, Dakatari huyo anasema mara nyingi mibinu hii ufanywa baada ya nusu saa ya mtoto kunyonyeshwa, na mtoto ulazwa kati ya mapaja alafu ndio mtoto anaanza kukandwa mgongoni ili kama kuna vihashilia vya hewa tumboni vitoke. Anasema njia hii itumike baada ya chakula kuanza kumeng’enywa tumboni ili mtoto asikitapike badala ya kutoa hewa (gas).
Kumnyonyesha mtoto kwa muda mfupi lakini mara kwa mara, anasema njia hii ni nzuri zaidi kwa watoto wanaokuwa na matatizo ya kupata hewa tumboni mara kwa mara kwani kwa kufanya hivyo kunaepusha kabisa hewa kuingia timboni.
“Mtoto ananyonya mara kwa mara lakini kwa muda mfupi. Mfano labda ananyonya dakika tano lakini kila baada ya nusu saa ananyonyeshwa tena. Maana mtoto akikaa kwenye ziwa muda mrefu anajiachia (ana relax) na kuachia mdomo wazi hivyo hewa inaingia ndani ya tumbo, lakini akinyonya kwa muda mfupi lakini mara nyingi unakuwa umemsaidia,”amesema
Njia nyingine ni kumlaza mtoto chali kisha kunyonga miguu kama kuendesha baskeli. Amesema njia hii pia inasaidia kutoa gesi tumboni.
Naye Muhudumu wa Afya ngazi ya jamii wa kituo cha Afya Nyanguge Joyce Nyanda amesema njia nyingine ya kumtoa mtoto hewa tumboni ni yakumuweka mtoto begani baada ya kumaliza kunyonya. Amesema mama ahakikishe tumbo la mtoto linagusa bega lake hapo ndipo mtoto atabeua na kutoa hewa tumboni.
Joyce amewataka wamama wenye watoto wachanga kuzingatia mikao wakati wakunyonyesha (possitions) akidai mara nyingi gesi huingia tumboni kwa sababu ya wanawake wengi kutozingatia mikao na mbinu ya unyonyeshaji.
Kesho tutaitafsiri kwa Kingereza. (Tomorrow we bring you the English version of this story so don’t miss out on this important information)