Maziwa ya mama hutoa kinga dhidi ya magonjwa mengi na ndio chanzo bora cha lishe kwa watoto wengi wachanga. Watoto wanaonyonyeshwa wana nafasi nzuri za kuishi na kufanikiwa. Katika muktadha wa COVID19, hakuna ushahidi kwamba ugonjwa unaweza kupitishwa kupitia maziwa ya mama, kwa hivyo mwongozo wa hivi karibuni ni kwamba wanawake walio na COVID-19 wanapendekezwa kuendelea kunyonyesha (kunyonyesha mapema pekee kutoka kuzaliwa hadi miezi 6 na kisha kuendelea hadi Umri wa miaka 2 na zaidi), lakini wanapaswa kuchukua tahadhari.
Ripoti inasema kuwa mama aliyethibitishwa kuwa na virusi vya Corona au anayeshukiwa kuwa na virusi hivyo anaweza kuendelea kunyonyesha na kwamba wanapaswa kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji na sabuni au dawa za kutakasa mikono kabla ya kumbeba au kumshika mtoto.
Pili avae barakoa ya kitabibu wakati akiwa amembeba au anamhudumia mtoto ikiwemo wakati anamlisha.
Tatu apigie chafya au akoholee kwenye kitambaa kisha anawe mikono na nne, asafishe eneo mara tu anapokuwa ameligusa.
Unyonyeshaji wa watoto wachanga ambao ni wagonjwa unapaswa pia kuendelea huku mama akichukua tahadhari zote za kiafya. Ikiwa mtoto mchanga hawezi kunyonyesha, msaidie mama aweze kumkamulia mtoto maziwa.
Kwa mama aliye na COVID-19 au shida zingine za kiafya, wanapaswa kuhimizwa na kuungwa mkono kukamua maziwa salama kwa mtoto, wakati wa kutumia hatua zinazofaa za usafi. Ikiwa mama anakamua maziwa yake kwa mkono au pampu ya matiti, anapaswa kunawa kabla ya kuguza matiti yake au kugusa pampu au sehemu za chupa na kuhakikisha kusafisha pampu kila baada ya matumizi. Akimaliza kumkamulia mtoto maziwa, mtu ambaya hana dalili za ugonjwa anaweza msaidia kumpa mtoto hayo maziwa yaliyokamuliwa na mama kwa kutumia kikombe safi na / au kijiko.
Source: UN News and Unicef