Kanuni ya afya inamtaka mama amnyonyesha mwanawe walau kwa kipindi cha miaka miwili.
Na katika kutumia maziwa hayo, kuna viasharia vya msingi kiafya vinavyosaidia kuonyesha yaliyojificha, iwapo mtoto ameshiba au bado ana haja ya kunyonya kutoka kwa mama yake.
Lakini, kuna ushauri wenye sura ya tahadhari kwamba iwapo mama ameathirika na Virusi vya Ukimwi (VVU) au madhara mengine yanayofanana na hayo.
Yanapokuwapo matatizo ya aina hiyo, inampasa mgonjwa amuone daktari kwa ufafanuzi zaidi juu ya hatua anazopaswa kuchukua.
Kilichomo kwenye unyonyeshaji
Wakati wa kunyonyesha kuna homoni inayojulikana kwa jina la ‘prolactin’ inayozalishwa mara tu mtoto anapoanza kunyonyeshwa na inasaidia kuongeza uzalishaji maziwa, huku ikizishusha chini homoni zinazohusiana na maandalizi ya yai la uzazi kwa mama huyo.
Ni jambo linalopunguza uwezekano wa mwanamke kupata ujauzito katika kipindi chote anachomnyonyesha mtoto wake kikamilifu.
Suala hilo linasababishwa na kukunjamana misuli ya kwenye matiti, inayochochewa na homoni ambayo kitaalamu inaitwa ‘oxytocin.’
Je, kuna umuhimu upi wa maziwa ya kwanza ya mama pale pindi tu unapomzaa mtoto, yaani colostrums?
Katika kipindi cha saa 24, mtoto anapokuwa amezaliwa, kuna kiwango cha wastani wa milimita 37 za lishe ya ‘colostrums’ inazalishwa kupitia maziwa hayo, ambayo yana protini pamoja na kinga kubwa dhidi ya magonjwa.
Hiyo ikilinganishwa na maziwa ya siku za baadaye, yasiyopatikana katika kundi lingine la maziwa, hapo inaingia maziwa ya kopo.
Sehemu ya maziwa ya kwanza kutoka kwa mama, yana kinga kubwa inayowasaidia watoto wachanga dhidi ya maradhi ya homa ya manjano na kuna zaidi ya aina 100 za virutubisho.
Kumyonyesha mtoto ndani ya miezi sita ya mwanzo, ni njia ya asili ya uzazi wa mpango, pia inawakinga kinamama kwa hatari ya kupata saratani ya matiti na kwenye yai la uzazi.
Tafiti za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinathibitisha endapo kila mtoto atanyonyeshwa maziwa ya mama ndani ya saa moja, baada tu ya kuzaliwa na kuendelezwa katika miezi sita ya mwanzo bila ya kula chochote mbadala, afya yake inakuwa imara, isipokuwa yanapokuwapo maagizo maalum ya kitabibu.
Unyonyaji huo unapaswa kuendelezwa hadi kufika umri wa miaka miwili, kwa kuchanganywa na lishe nyinginezo baada ya hapo.
Hatua hizo bora zinapofuatwa kwa kuzingatia miongozo sahihi ya kiafya, inaelezwa kuepusha vifo vingi vinavyokadiriwa kufika wastani wa watu 800,000 kila mwaka nchini.
Namna ya kunyonyesha
Mtoto anapaswa kunyonyeshwa kila baada ya saa moja hadi tatu, lakini kunyonyesha huko kunapaswa kuendane na dalili za njaa na si kuzingatia kanuni ya muda peke yake.
Kunyoshesha kupitiliza kiasi, bila ya kuzingatia dalili za shibe kwa mtoto, inaweza kuzuia maziwa yasifike tumboni, yanarudi mdomoni. Ni hali inayoitwa kitaalamu ‘gastro esophageal reflux disease.’
Faida maziwa ya mama
Kiafya, faida ni nyingi zitokanazo na maziwa ya asili ya mama, pindi anapopewa mtoto. Mosi, inamkinga dhidi ya maradhi ya mfumo wa chakula yanayoweza kudhuru utumbo mkubwa na mdogo.
Pili, watoto wanaopata maziwa asili ya mama, wana kinga dhidi ya maradhi ya sikio pumu na magonjwa ya ngozi (eczema).
Tatu, watoto hao wapo katika kinga ya kupata utapiamlo na hasa unaoambatana na kuongezeka uzito pamoja na kisukari cha ukubwani.
Mwisho, maziwa ya asili yanamuimarisha mama na mfumo wake wa fahamu kwa mtoto.
Kwa muda wa miezi sita kikamilifu mtoto anatakiwa kupewa maziwa ya mama tu. Vinywaji kama Oral rehydration solution (ORS), Vitamin na dawa kutoka na maagizo ya daktari mhusika.
Mtoto anatakiwa kunyonyeshwa kila baada ya saa moja hadi tatu, lakini kunyonyesha huku kuambatane na dalili za njaa tu na sio kwa kuzingatia saa.
Kunyoshesha kupitiliza kiasi bila kuzingatia dalili za kushiba kunaweza kusababisha maziwa kutofika tumboni hivyo kurudi mdomoni (gastroesophageal reflux disease).
Maziwa ya kopo
Inaelezwa kuwa mapungufu yaliyomo katika maziwa ya kopo ni kwamba yamekosa protini zinazopigana na magonjwa.
Ni hali inayowaweka watoto wasiopata maziwa ya mama katika hatari kiafya, kwa kuwa karibu na maradhi kama vile homa ya mapafu, kwani hawana kinga ya kutosha kusogeza mbali baadhi ya maradhi.
Pia, baadhi ya wazazi na walezi wanapunguza gharama kwa huchanganya maziwa hayo na kiwango kikubwa cha maji, ili yasitumike maziwa mengi ambayo wameyanunua kwa bei kubwa.
Matokeo ya mfumo huo wa lishe inamfanya ashibe, pasipo kupata manufaa makubwa kiafya kama vile kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.
Ilivyo njaa, shibe
Kuna viashiria kadhaa vya njaa kwa mtoto mchanga: Anaweka kidole mdomoni; anazungusha kichwa kulitafuta ziwa; analia; anajinyoosha; na kupiga mihayo.
Mengine ni kufungua mdomo na kutoa ulimi nje; kunyonya kitu chochote kilicho karibu yake; anageuza kichwa kila upande; pia mikono na miguu anaipeleka mdomoni.
Pia, mtoto anaposhiba ana viashiria vyake. Kwa kawaida mtoto aliyeshiba anashikwa na usingizi; mwili unalainika; na anajinyoosha.
Namna ya kunyonyesha
Mtoto anapaswa kunyonyeshwa kila baada ya saa moja hadi tatu. Lakini unyonyeshaji huo unapaswa uendane na dalili za njaa na si kuzingatia muda peke yake.
Kunyoshesha kupita kiasi bila ya kuzingatia dalili za shibe kwa mtoto, inaweza kusababisha maziwa yasifike tumboni huwa yanarudi mdomoni. Ni hali inayoitwa kitaalamu ‘gastro esophageal reflux disease.’
Jinsi ya kumnyonyesha mtoto, mdomo unatakiwa kuwa wazi na sehemu ya juu ya chuchu ya titi inaonekana, ikilinganishwa na chini.
Aidha, inatakiwa kusikika kwa sauti za kumeza bila kugota, mashavu ya mtoto yanakuwa duara bila ya mbonyeo na mienendo mbalimbali ya taya.
Watoto wao hawahitaji virutubisho vya kinga na kujenga mwili vya vitamin D kutoka hospitali, ili kuwaepusha na ugonjwa wa matege.
Maziwa hayo ya mama yanaelezwa kuwa, maziwa hayo ya mama yana kiwango bila ya kufuata taratibu za kiafya.
VVU na unyonyeshaji
Takwimu zinaonyesha kuwa awali kati ya asilimia tano na 20 ya watoto waliozaliwa na mama waathirika wa virusi vya Ukimwi, nao walipata VVU kupitia unyonyeshaji.
Hata kwa kuzingatia dawa za kupunguza makali ya VVU, asilimia hiyo inapungua hadi kufikia tatu. Kudumu kwa kiwango hicho au kupungua zaidi ni kwamba, jamii inayoguswa na kanuni hizo inapaswa kuzingatia kanuni za afya zilizopo katika mustakabali wa unyonyeshaji.
Ushauri kwa kinamama wenye VVU bila ya kutumia dawa, ni kwamba wanapaswa kuanza kuzitumia dawa hizo za kupunguza makali ya VVU na wakati huohuo kuchukua tahadhari katika namna ya kunyonyesha watoto wake.
Mfano mdogo uliopo ni kwamba, mama huyo mzazi akiwa hata na mkwaruzo kwenye chuchu la titi lake, basi atumie lingine kunyonyesha mtoto.
Pia mwongozo wa kiafya uliopo ni kwamba, mama mnyonyeshaji hapaswi kutumia dawa pasipo ushauri kutoka kwa daktari, kwani zinaweza kuwa na madhara kwa mtoto wakati anamnyonyesha.
Matatizo
Matatizo yanayoweza kutokea katika muda wa kumnyonyesha mtoto, kama vile maumivu katika chuchu yanayosababishwa na maradhi ya matiti pamoja na matatizo ya kimaumbile ya ulimi wa mtoto.
Hivyo, inampasa mgonjwa umuone daktari kwa ushauri wa kitabibu, kuwezesha unyonyeshaji kuendelea kama kawaida.
Maradhi yanayomhusu mtoto, ni kama vile maradhi ya fangasi mdomoni katika hali usiache kunyonyesha mtoto, matatizo katika maumbile ya ulimi.
Kutonyonyesha
Mama anayenyonyesha, anashauriwa kula baadhi ya vyakula kama vile papai, karoti, spinachi, supu ya ng’ombe, parachichi, ndizi, mafuta ya nazi, mtindi na uji wa ulezi wenye virutubisho.
Mwandishi wa makala hii mwanafunzi wa taaluma ya tiba na anapatikana kwa mawasiliano ya simu: +255 759 775788
Source: Nipashe
1 Comment
Please tell me that youre heading to keep this up! Its so great and so important. I cant wait to read more from you. I just really feel like you know so considerably and know how to make people listen to what youve to say. This weblog is just also cool to become missed. Terrific stuff, actually. Please, PLEASE keep it up!