Kula angalau milo 3 iliyo kamili na asusa (vitafunwa) kwa siku.
Chagua vyakula kutoka kila kundi katika makundi yafuatayo:
Wakati ukiwa mjamzito au unanyonyesha mwili wako unahitaji mlo kamili ambao hutokana na kula vyakula vya aina mbalimbali. Vyakula
mbalimbali kila siku husaidia kuhakikisha kuwa unapata nishati na virutubishi vyote vinavyohitajika mwilini mwako pamoja na mahitaji
ya mtoto.
Lishe bora hukusaidia:
Kuongezeka uzito angalau kilo 12 wakati wa ujauzito. Uzito huongezeka wastani wa kilo moja kwa mwezi.
✽ Kuzuia upungufu wa damu.
✽ Kuboresha ukuaji na maendeleo ya mtoto wako.
✽ Kuutayarisha mwili wako kunyonyesha. Mahitaji ya nishati na virutubishi wakati wa kunyonyesha ni makubwa kuliko wakati wa
ujauzito.
✽ Kupunguza uwezekano wa kujifungua kabla ya wakati, mtoto
mwenye uzito pungufu, au mfu.
Wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wanahitaji
✽ Kuongeza kiasi cha chakula kwa mlo au kula milo midogo mara nyingi.
✽ Kula asusa kati ya mlo na mlo.
✽ Kula matunda na mbogamboga kwa wingi
katika kila mlo.
✽ Kunywa maji ya kutosha kila siku (glasi 8 au lita 1.5).
✽ Kuepuka kunywa chai au kahawa pamoja na mlo, kwani huzuia usharabu wa madini ya chuma na huweza kuchangia katika kuleta
upungufu wa damu. Ni vyema kunywa chai au kahawa saa moja kabla au baada ya kula chakula
Je, unahitaji virutubishi gani vya nyongeza?
Kipindi chote cha ujauzito na hadi miezi mitatu baada ya kujifungua unahitaji vidonge vya madini ya chuma na vya
foliki asidi kuzuia upungufu wa damu.
Ni vyema kumeza vidonge vya madini ya chuma pamoja na chakula ili kuongeza usharabu na kupunguza athari kama
kichefuchefu.
✽ Daima tumia chumvi yenye madini joto kwenye chakula ili kuzuia upungufu wa madini joto mwilini.
✽ Tumia virutubishi vya nyongeza vya vitamin A mara baada ya kujifungua au katika kipindi cha wiki 4-6 kama utakavyoelekezwa
na mhudumu wa afya. Vitamin A husaidia kujenga mfumo wa kinga ya mwili wa mtoto wako.
✽ Daima fuata maelekezo unayopewa na wahudumu wa afya
Source: URC
Link: https://www.urc-hs.com/sites/default/files/Nutrition_during_pregnancybreastfeeding-SWA.pdf