Uzazi wa mpango ni uamuzi wa hiari unaofanywa na mtu binafsi, mke/mume/
mwenzi/kijana katika kupanga ni lini wapate watoto, idadi ya watoto, baada ya muda
gani na njia ipi ya uzazi wa mpango wangependa kutumia. Hata wakati unanyonyesha, kuna aina mbali mbali za njia za uzazi wa mpango na njia hizo ni vidonge, sindano, mipira ya kike na kiume, vipandikizi, kitanzi, upasuaji mdogo, kutofanya ngono na pia njia za asili kama vile
kalenda n.k. Uzazi wa mpango pia unajumuisha taarifa kuhusu namna ya kushika
mimba inapohitajika na kutibu ugumba.
Uzazi wa mpango wa hiyari
Utaratibu wa Uzazi wa Mpango kwa hiyari unawawezesha wanawake na wanaume
kunufaika na haki yao ya uzazi kwa kuamua kwa hiyari yao ni lini wapate watoto,
idadi ya watoto, baada ya muda gani na njia ipi ya uzazi wa mpango wangependa
kutumia. Uzazi wa mpango ni haki ya msingi ya binadamu na haihusiani na dhana
potofu kwamba zinalengo la kudhibiti idadi ya watu.
Source: UNFPA TANZANIA