Anza kumpa mtoto chakula cha nyongeza anapotimiza miezi 6
Nini:
Uji au chakula kilichopondwa vizuri
Mara ngapi:
Mara 2 kila siku
Kiasi gani:
Mlishe vijiko vya chakula 2-3 kila mlo
Umri wa miezi 7 – 8
Nini:
Chakula kilichopondwa
Mara ngapi:
Mara tatu kwa siku
Kiasi gani:
Mlishe theluthi mbili (2/3) ya kikombe
kila mlo (kikombe 1=mls 250)
Umri wa miezi 9 – 12
Nini:
Chakula kilichokatwa vipande vidogo
vidogo au kilichopondwa na vile ambavyo
mtoto anaweza kushika mwenyewe.
Mara ngapi:
Mara 3 kila siku pamoja na asusa moja.
Kiasi gani:
Mlishe robo tatu (3/4) ya kikombe kila
mlo (kikombe 1=mls 250)
Umri wa miezi 12 – 24
Nini:
Vyakula vinavyoliwa na familia, vikatwekatwe au kuponda kama inahitajika.
Mara ngapi:
Mara 3 kila siku pamoja na asusa mbili
Kiasi gani:
Mlishe kikombe kilichojaa kila mlo
(kikombe 1=mls 250)
KUMBUKA:
✽ Kati ya umri wa miezi 6 na miaka 2 mtoto bado huhitaji maziwa ya mama kila siku ili kupata
nishati na virutubishi muhimu. Kama mtoto hanyonyeshwi atahitaji kikombe 1 au 2 vya maziwa mengine kila siku mpaka atimize miaka miwili au zaidi. Kama maziwa hayapatikani mpe mtoto milo miwili ya ziada.
✽ Epuka kumpa mtoto vinywaji ambavyo havina virutubishi kwa mfano chai, kahawa, soda na
vinywaji vya rangi na sukari (juisi bandia). Mpe mtoto maji ya matunda halisi (juisi) kwa kiasi.
✽ Maziwa freshi ya wanyama na maji anayopewa mtoto lazima yachemshwe. Mpe mtoto maji
safi na salama kila siku kukidhi kiu yake.
✽ Daima tumia kikombe kilicho wazi kumlishia mtoto. Usitumie chupa au vikombe vyenye mifuniko yenye vitundu vidogo kwani ni vigumu kuvisafisha.
✽ Kuongezeka uzito ni kiashiria cha afya bora na hali nzuri ya lishe. Endelea kumpeleka mtoto kwenye kliniki ya watoto kila mwezi ili kuchunguza afya, kupata chanjo na kufuatilia ukuaji na maendeleo yake.
✽ Mtoto akiwa mgonjwa apewe milo midogo mara kwa mara pamoja na vinywaji kwa wingi ukijumuisha maziwa ya mama.
Mhimize mtoto ale vyakula vya aina mbalimbali hasa vile ambavyo anavipendelea. Mara mtoto apatapo nafuu au kupona ongeza kiasi cha chakula na idadi ya milo.
Source: Ilichapishwa kwanza na URC-CHS
Both technical and financial support for the development of the brochure where we got the content was provided by the Quality Assurance Project (QAP), managed by University Research Co., LLC (URC), under USAID
Contract Number GPH-C-00-02-00004-00. September 2005
Link: https://www.urc-chs.com/file/1399/download?token=gaS0Sk7y