Kila mara ni bora kupatiana ushauri kuhusu ulishaji wa mtoto mchanga kabla ya kuzaliwa na pia kuendelea kusisitiza baada ya kipindi cha kuzaliwa. Mafunzo haya lazima yaangazie kuhusu uanzishaji na udumishaji wa unyonyeshaji bora. Utaratibu wa kupata haya yameandikwa kama yafuatayo:
Utaratibu wa unyonyeshaji bora
Anza kunyonyesha baada ya saa moja ya kuzaa (unyonyeshaji wa mapema)
Usimptie mtoto chochote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza (unyonyeshaji wa kipekee)
Usimwage maziwa ya kwanza ya mama baada ya kuzaa, huwa na protini na kingamwili ambayo ni muhimu kwa mtoto mchanga. Unapaswa kumwambia mama amlishe nayo mtoto mchanga, kwa sababu ni ‘chanjo’ ya kwanza ambayo mtoto atapata.
Keti kwa hali nzuri wakati unanyonyesha
Hakikisha mtoto anapata vizuri matiti ya mama anaponyonya
Hakikisha mtoto ananyonya vizuri
Unapomtembelea baada ya kipindi cha kuzaa, mwambie mama amweke mtoto kwa matiti ili ukague namna anavyompatia matiti na anavyonyonya (tunaelezea jinsi ya kufanya hivyo katika sehemu inayofuata). Ikiwa mtoto alikuwa amelishwa hivi karibuni, ngojea angalau saa moja kabla ya kumpatia maziwa ya matiti tena. Hii itakupatia fursa ya kuchunguza jinsi mtoto anavyonyonya na kuweza kubaini iwapo kuna matatizo yoyote ya kunyonya, ambayo unaweza kumsaidia mama kutatua. Kabla ya kuondoka hakikisha kwamba mama anaelewa jinsi ya kunyonyesha mtoto wake kwa njia inayofaa.
7.1.1 Ishara nne nzuri za mama kukaa
Jambo la kwanza ni mama kuketi kwa utulivu na kudumisha ishara nne nzuri za kuketi
Kichwa na mwili wa mtoto mchanga uwe laini
Mtoto mchanga atazame matiti yake na pua lake liwe kinyume cha chuchu
Mwili wa mtoto mchanga iwe karibu na ya mama
Mama anashikilia mwili wote wa mtoto bali sio shingo na mabega.
Source: https://www.open.edu/openlearncreate/mod/oucontent/view.php?id=53442&printable=1
1 Comment
Oh my goodness! a tremendous article dude. Thanks However Im experiencing subject with ur rss . Don’t know why Unable to subscribe to it. Is there anybody getting identical rss downside? Anyone who is aware of kindly respond. Thnkx Have you considered promoting your blog? add it to SEO Directory right now 🙂