Mama anapougua (1), chembe chembe nyeupe mwilini mwake hutengeneza
‘kingamwili’ zitakazopigana na ugonjwa na kumlinda
(2). Baadhi ya chembe chembe
nyeupe huenda kwenye matiti na kutengeneza ‘kingamwili’
(3) ambazo zinapatikana
kwenye maziwa na kumkinga mtoto wake
(4).
Hivyo mama anapokuwa mgonjwa asitenganishwe na mtoto wake kwani maziwa yake
yanamlinda mtoto dhidi ya maradhi.
□ Maziwa mbadala hayana chembe hai. Maziwa haya hayana chembe chembe nyeupe
au ‘kingamwili’ wala viini vingine vya kumkinga mtoto na magonjwa
□ Katika mwaka wa kwanza wa mtoto, mfumo wa kinga ya maradhi unakuwa haujakomaa,
hivyo hauwezi kukabiliana na maradhi kama ule wa mtoto mwenye umri mkubwa au
mtu mzima. Hivyo mtoto anahitaji kulindwa na mama yake kupitia maziwa yake.
□ Maziwa ya mama yana chembe chembe nyeupe za damu na viini vingi vinavyomkinga
mtoto na maradhi pamoja na kingamwili dhidi ya magonjwa aliyougua mama.
Tofauti kati ya maziwa ya mwanzo ya manjano na yale yanayotoka
baadaye
� Virutubisho vilivyomo katika maziwa ya mama, wepesi au uzito wa maziwa hubadilika
kutokana na umri wa mtoto na hatua ya kunyonya. Pia tofauti hiyo hutegemea muda
mtoto anaotumia kunyonya.
� Maziwa ya mwanzo yenye rangi ya njano hutoka siku tatu za mwanzo baada ya mama
kujifungua. Baada ya siku chache maziwa ya mama huwa meupe na kutoka kwa
wingi, matiti hujaa na kuwa mazito.
� Mtoto anaponyonya maziwa yanayoanza kutoka huwa ya maji maji na anapoendelea
kunyonya maziwa huwa meupe zaidi na mazito.
Source: Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TNFC)
Link: https://www.tfnc.go.tz/uploads/publications/sw1515868144-Kitabu%20Cha%20Mkufunzi-Mafunzo%20kwa%20Wanasihi.pdf
2 Comments
Your point of view caught my eye and was very interesting. Thanks. I have a question for you. https://accounts.binance.com/tr/register-person?ref=OMM3XK51
You can ask your question.