MAMA
: Mama anaonekana mwenye afya njema
Mama ametulia na ana raha
Dalili za uhusiano kati ya mama na mtoto
MTOTO
Mtoto anaonekana mwenye afya njema
Mtoto ametulia na ana raha
Mtoto anatafuta titi kama ana njaa
MATITI
Matiti yanaonekana yenye afya
Hakuna maumivu au kujisikia vibaya
Matiti yameshikiliwa vizuri bila kubana chuchu
MTOTO ALIVYOPAKATWA
Mwili wa mtoto umenyooka
Mwili wa mtoto umesogezwa karibu na mama
Mwili wote wa mtoto umeshikiliwa
Uso wa mtoto unaelekea kwenye titi la mama
MTOTO ALIVYOWEKWA KWENYE TITI
Sehemu nyeusi ya titi inaonekana zaidi juu ya kinywa cha mtoto
Kinywa cha mtoto kimeachama vya kutosha
Mdomo wa chini umebinuka nje
Kidevu cha mtoto kinagusa titi
KUNYONYA
Mtoto ananyonya taratibu, akigugumia na kupumzika
Mashavu ya mviringo wakati wa kunyonya
Mtoto anaachia titi anaposhiba
Mama anagundua dalili za kisohiari cha oksitosini
Source: Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC)