- Maziwa ni lazima yakamuliwe na kuhifadhiwa katika hali ya
usafi.
- Maziwa haya yanaweza kuhifadhiwa kwenye jokofu
(refrigerator) kwa muda wa siku nne. Yasipowekwa kwenye
jokofu maziwa yatumike ndani ya masaa 4 mpaka 8. - Maziwa yanaweza kugandishwa kwenye ‘freezer’ na
kuhifadhiwa humo kwa muda wa miezi 4 mpaka 6. - Unapohifadhi maziwa kwa kugandisha yatunze kwenye
vyombo (containers) ndogo ndogo (200 – 350 mls) na
hakikisha unabandika tarehe uliyokamua katika kila
chombo. - Anza kutumia maziwa ya zamani kwanza kabla ya mapya
kulingana na tarehe uliyobandika. - Maziwa yaliyoganda yakitolewa kwenye freezer na
kuyeyushwa, yasigandishwe tena. Maziwa haya yanaweza
kutunzwa kwenye jokofu kwa siku 4 zaidi. - Pasha maziwa kiasi anachohitaji mtoto kabla yakumpatia
kwa kutumia maji ya moto. Maziwa haya hayahitaji
kuchemshwa. - Maziwa haya ni bora kwa lishe ya mtoto sawa sawa na
mtoto anaponyonya moja kwa moja kwenye ziwa la mama. - Njia hii ya lishe inaboresha afya ya mtoto na mama na
hupunguza gharama za malezi (Pesa nyingi ambazo
zingetumika kununua maziwa ya kopo ambayo ubora wake
hauna uhakika).
10.Zingatia usafi wakati wa kukamua na kuhifadhi maziwa. - Pamoja na kwenda kazini/chuoni wewe pia unaweza kumnyonyesha mtoto wa wako maziwa yako tu mpaka miezi sita. Zingatia na tia nia.
- Source: MUHAS
- Link: https://hesperian.org/wp-content/uploads/pdf/sw_hmx/sw_breastmilkinfo_HelenMtui_2014.pdf