Inaweza kumchukua mama dakika 20-30 kukamua maziwa ya titi, au hata muda zaidi mwanzoni, lakini mama huongeza kasi ya kukamua pindi anavyopata uzoefu. Kwanza mshauri mama anawe mikono na kuosha matiti kwa sabuni na maji, kisha aikaushe kwa taulo taulo safi kabisa. Kiandae kikombe safi kilichochemshwa au chupa iliyo na mdomo mkubwa. Iwapo hawezi kuchemsha kikombe chote, kitie maji yanayochemka na uyaache mle hadi muda mchache kabla ya kutia maziwa. Kisha yamwage yale maji. Maziwa hukingwa dhidi ya bakteria kwa kufanya hivi.
Mama anafaa kuketi vyema kisha aegemee kikombe.Finya nyuma kidole gumba na vidole vingine kuelekea kifuanikisha ukizungushe kidole gumba kwenda mbele kana kwamba unatolesha alama za kidole. Hii ni ili kuyatoa maziwa kutoka sehemu zote za titi. Kamua titi moja kwa angalau dakika 3 – 4 hadi maziwa yapungue, kisha ukamue hilo lingine. Kuwaza kuhusu mtoto wake anapokamua kunaweza kufanya maziwa yachuruze kwa urahisi zaidi.
Source: Open University
Link: https://www.open.edu/openlearncreate/mod/oucontent/view.php?id=53443§ion=1.5.3