By Lizzy Masinga
Wataalamu wa afya wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa watoto wachanga kupata lishe bora ya maziwa ya mama tangu muda mfupi tu baada ya kuzaliwa.
Maziwa ya mama humpatia mtoto virutubisho vyote anavyohitaji katika miezi 6 ya mwanzo toka kuzaliwa, lakini suala la Imani potofu miongoni mwa jamii limekuwa likikwamisha watoto wachanga kupata lishe bora inayostahili.
Daktari bingwa wa watoto, Pius Muzazi anasema pamoja na umuhimu wa kunyonyesha mara tu mtoto anapozaliwa, kuna imani potofu nyingi zilizo miongoni mwa jamii kuhusu masuala ya unyonyeshaji, hali inayofanya watoto wachanga wasipate lishe inayostahili na kuathiri afya zao.
Maziwa ya kwanza ya rangi ya manjano si mazuri kwa mtoto?
Kumekuwa na mtazamo kuwa maziwa ya kwanza ambayo mama huyapata mara baada ya kujifungua si maziwa yafaayo kwa mtoto, wanawake wengine huyakamua na kuyamwaga mpaka yanapotoka maziwa ya rangi nyeupe kuna ukweli kuhusu hilo?
Daktari: Maziwa ya kwanza ya mama kwa kitaalamu huitwa colostrum hii colostrum ndio maziwa muhimu zaidi kuliko maziwa yoyote yale mama atakayokuja kuyatoa.
Haya ni maziwa ya kwanza ambayo huwa kama chanjo ya kwanza kabisa kwa mtoto, kwanza yana virutubisho vingi na pia yana kinga ambazo yatamsaidia mtoto kutokupata maradhi mbalimbali huko mbele.
Kukamua maziwa ya kwanza ni kama kutupa dhahabu
Wakina mama hufikiri kuwa hawana maziwa ya kutosha
Wanawake huwa wanapata wasiwasi watoto wao wanapokuwa wakilia wakihisi kuwa hawana maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wao.Je ni kweli kuwa maziwa ya baadhi ya wanawake hayatoshi?
Daktari:Kwanza kuhusu kutosha au kutokutosha kwa maziwa ya wakina mama, tafiti zinaonesha kuwa ni asilimia kubwa ya wakina mama maziwa yao yanatosha kabisa.
Tatizo lililopo hapa ni kuwa kina mama wengi wanafikiri kuwa hawana maziwa ya kutosha kwasababu utengenezaji wa maziwa pia unahusisha saikolojia ya mama mwenyewe, kama una mawazo mengi, msongo wa mawazo, umechoka basi utoaji wa maziwa utapungua na ndio maana wakinamama wengi wanakuwa hawatoi maziwa ya kutosha.
Lakini na pia tunasahau kuwa unyonyeshaji si wa mama peke yake, suala la unyonyeshaji linahusisha mama na baba pia, hivyo mama anahitaji sana kusaidiwa na baba ili maziwa yatoke kwa wingi.
Kusema kuwa maziwa hayatoshi ni imani potofu
Ni kweli mtoto mchanga anahisi kiu?
Baadhi ya wanawake huwapa watoto maji kwa kijiko wakifikiri watoto wana kiu kwasababu wamenyonya maziwa kwa muda mrefu.
Daktari: Maziwa ya mama yana virutubisho vyote muhimu ikiwemo maji, mtoto anayenyonya ndani ya miezi sita hahisi kiu hivyo asipewe maji.
Mtoto akilia sana maana yake hashibi?
Daktari: Mtoto anaweza kulia kwa sababu nyingi sana, lakini mama akimnyonyesha, kunyonyesha kwenyewe kunaweza kutumika kama njia ya kumbembeleza mtoto, tumezungumza kuhusu maziwa kuwa mengi, kama mama atafuata maelekezo yote maziwa yake yatatosha na mtoto atashiba vizuri, lakini pia ni vizuri kujua sababu nyingine za mtoto analia.
Baba na mama wa mtoto hubemenda mtoto?
Ni kweli baba na Mama wa mtoto hawawezi kujamiiana wakati mtoto anapokuwa bado ananyonya?
Daktari: Kuna imani kuwa lazima mama aoge ajisugue na sabuni kwanza kabla ya kunyonyesha kwa hofu ya kumharibu mtoto, hii si kweli kwani mtoto anaweza kunyonya wakati wowote ule
Maziwa ya mama huchacha ndani ya mwili ?
Mfano mama anaweza kusafiri kwa kipindi fulani akirejea hukamua kwanza maziwa kwa kuwa maziwa yamechacha je ni kweli?
Source: This article was published by BBC
Link: https://www.google.com/amp/s/www.bbc.com/swahili/habari-58097699.amp