Kumekuwa na mtazamo kuwa maziwa ya kwanza ambayo mama huyapata mara baada ya kujifungua si maziwa yafaayo kwa mtoto, wanawake wengine huyakamua na kuyamwaga mpaka yanapotoka maziwa ya rangi nyeupe kuna ukweli kuhusu hilo?
Daktari: Maziwa ya kwanza ya mama kwa kitaalamu huitwa colostrum hii colostrum ndio maziwa muhimu zaidi kuliko maziwa yoyote yale mama atakayokuja kuyatoa.
Haya ni maziwa ya kwanza ambayo huwa kama chanjo ya kwanza kabisa kwa mtoto,kwanza yana virutubisho vingi na pia yana kinga ambazo yatamsaidia mtoto kutokupata maradhi mbalimbali huko mbele.
Source: BBC
Link: https://www.bbc.com/swahili/habari-58097699